KARIBU

UMEME SACCOS LIMITED

Historia ya Chama

Umeme Saccoss ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha wafanyakazi waajiriwa wa kudumu na Muda maalumu (TMP) wa shirika la Umeme Tanzania TANESCO. Ushirika huu ulianzishwa rasmi mnamo Mwaka 1999 ukiwa na wanachama wapatao 50. Ushirika huu umesajiliwa kwa mujibu wa sheria Ushirika namba 15 ya mwaka 1991 fungu la 30 na kupata Hati ya usajili mnamo Tarehe 18/3/1999 yenye namba-MBR 445.

Dira ya Chama ni Kuwezesha kukuza Ushirika wa Akiba na Mikopo unaotoa huduma bora za kifedha ambazo ni nafuu, rahisi zinazokidhi na kuridhisha kwa wanachama na jamii kwa ujumla.

Kujiunga na Chama

Mtumishi yeyote wa Shirika la umeme nchini Tanzania (TANESCO) na mweza (MKE/MME) wanaweza kujiunga na chama hiki. Kiingilio cha kujiunga uanachama ni Tshs 100,000/=. Baada ya kujiunga mwanachama anaanza kuweka akiba, amana na pia kununua hisa kidogo kidogo au kwa mkupuo kadiri ya uwezo wake mpaka atakapomaliza Idadi ya hisa zote zinazohitajika kwa ajili ya umiliki wa chama na atakapomaliza atapatiwa Cheti Cha Umiliki wa Hisa UMEME SACCOS LTD.

Umeme Saccos

Pata taarifa zako Kiganjani

Chama kina Programu ya Simu ya Mkononi yaani "Mobile app" ambapo wanachama wataweza kuingia kwenye mtandao na kupata taarifa zake.

Mwanachama atawezeshwa kupakua app hiyo kupitia Playstore na kupata statement zake za mikopo na michango.

Pata taarifa zako Kiganjani

Chama kina Programu ya Simu ya Mkononi yaani "Mobile app" ambapo wanachama wataweza kuingia kwenye mtandao na kupata taarifa zake.

Mwanachama atawezeshwa kupakua app hiyo kupitia Playstore na kupata statement zake za mikopo na michango.

0

Miaka ya Huduma

0 +

Wanachama

0 +

Bidhaa za Mikopo

0 +

Matawi

Kikokotoo cha Mkopo

Ingiza Taarifa za Mkopo
Jumla ya Riba
Gharama za Mkopo
Kiasi Jumla
Mkopo + Riba
Malipo ya Mwezi
kwa mwezi
Jedwali la Malipo (Salio Pungufu)
MweziMalipo ya MweziSehemu ya MkopoSehemu ya RibaMkopo Uliosalia
JUMLA

Ushuhuda wa Wateja

Pongezi kwa chama chetu cha Umeme Saccos kwa kutoa huduma bora na kutujali sisi wanachama wake, kwani wanatoa suluhisho la changamoto yoyote pale mwanachama wake wake anapohitaji huduma, Umeme Saccos huduma bora, huduma safi wakati wowote.

Bakari Mwikola Mwanachama

Napenda kutoa shukran zangu na pongez Kwa Umeme Saccos Kwa kutoa huduma vizuri Kwa wanachama na kwa haraka.Nimenufaika na chama hiki tangu nilipojiunga nimepata huduma nzuri na zenye tija kwangu na watu wanao nitegemea.

Josam Issa Mwanachama

Najivunia sana kuwa mwanachama wa Umeme Saccos sababu imekuwa msaada mkubwa katika kuendelea na kuendesha maisha yangu na pia ni sehemu sahihi na salama kwa uhakika wa kujiwekea akiba, amana na huduma zingine zote zinazotolewa na Umeme Saccos.

Sharifa Komba Mwanachama

Najivunia kuwa miongoni mwa wanachama wa Umeme Saccos, zipo sababu nyingi sana zinazofanya nijivunie moja ni kunipa mkopo kwa haraka na wakati wakati huo riba ya mkopo ni ndogo sana. Kila mrejesho na kikao nashiriki kwa ajili ya kufahamu taarifa na maendeleo ya chama chetu.

Stanley Msoloka Mwanachama

Wadau Wetu