Historia ya Chama

  1. Home
  2. »
  3. Historia ya Chama

UMEME SACCOS LIMITED ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha wafanyakazi waajiriwa wa kudumu na Muda maalumu (TMP) wa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Ushirika huu ulianzishwa rasmi mnamo Mwaka 1999 ukiwa na wanachama wapatao 50, Na wakati unaanzishwa ulitambulika kwa jina la TANESCO MBEYA SACCOS. Baada ya chama hiki kusambaa mikoa yote ya Tanzania ndipo jina likabadilishwa mnamo mwaka 2026 na kuanza kuitwa UMEME SACCOS. Ushirika huu umesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya Vyama Vya Ushirika namba 15 ya mwaka 1991 fungu la 30 na kupata Hati ya usajili mnamo Tarehe 18/3/1999 yenye namba PRI-MBY-MBY-CC-2022-2349

Kufuatana na mabadiliko ya mara kwa mara ya sheria ya vyama vya ushirika hivi sasa chama kinafanya shughuli zake chini ya Sheria ya vyama vya ushirika Na.6 ya Mwaka 2013 na kanuni za SACCOS za mwaka 2015.
Mnamo mwezi January mwaka 2021 Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Umeme Saccos kilipewa leseni ya utoaji wa Huduma ndogo za fedha Namba MSP3-TCDC/2021/0041 Chini ya kifungu namba 20 cha sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018.