Mkopo wa sikukuu ni kwa kila mwanachama ambaye anataka kujiandaa vema wakati wa maandalizi ya sikukuu au sherehe za aina zote kubwa na ndogo kama vile sherehe za siku za kuzaliwa, sherehe za maadhimisho ya familia, kitaifa na kimataifa. Vile vile sherehe za mwanachama kujipongeza katika mambo mbalimbali ya binafsi. Mkopo huu kiwango cha mwisho ni Tsh 500,000 na unalipwa ndani ya awamu mbili (2). Mkopo wa sikukuu hauzingatii Akiba za mwanachama wakati wa kukopa.