Bodi ya chama inawatangazia wanachama wote wawakilishi ambao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama, kwamba Mkutano Mkuu wa 22 wa Mwaka 2026 utafanyika Mbeya tarehe 24 Oktoba 2026 katika ukumbi wa TUGHIMBE HALL kuanzia saa 02:00 asubuhi.
AGENDA ZA MKUTANO MKUU WA 22:
1. Kuthibitisha Akidi. 2. Kufungua Mkutano. 3. Kuchagua Mwenyekiti wa Mkutano. 4. Kusoma na kuthibitisha Muhtasari wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa 21 wa Mwaka 2025 na yatokanayo na Mkutano Mkuu wa mwaka wa 2025. 5. Kupokea na Kuidhinisha wanachama wapya . 6. Kupokea Taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya chama. 7. Kupokea Taarifa ya kamati ya Usimamizi. 8. Kupokea na kuthibitisha Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za mwaka 2025 (COASCO) 9. Kupokea, kujadili na Kuidhinisha Mpango Kazi na Makisio ya Mapato na Matumizi ya mwaka 2027. 10. Dondoo 11. 12. 13. Uchaguzi. Mengineyo. Kufunga Mkutano. Ninawatakia wajumbe wote maandalizi mema na ushiriki mzuri wa Mkutano huo pamoja na mwisho wa mwaka wenye Amani.
MUHIMU Taarifa zote zitakuwa kwenye kalablasha la mkutano na litatoka siku saba (7) kabla ya Mkutano mkuu, hivyo uongozi unawahimiza wawakilishi kulisoma na kulielewa kikamilifu ili kusaidia kujenga hoja. Hakutakuwa na kusoma kalablasha neno kwa neno badala yake hoja zitapokelewa ili kujibu hoja. Lengo ni kukomboa muda kwa kuwa kuna matukio mengi.