Uongozi wa UMEME SACCOS Ltd unapenda kuwatangazia Wanachama na Wajumbe Wawakilishi wenye sifa za kugombea nafasi za Uongozi ndani ya Chama kwamba, fomu zitaanza kutolewa kuanzia tarehe 01/09/2026 hadi 16/10/2026.
1. Wajumbe wa Bodi – Nafasi 9
2. Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi – Nafasi 3
Fomu hizo zitapatikana katika, Ofisi za UMEME SACCOS, zilizopo Mtaa wa Sokomatola Barabara ya 3 Mkabala na ukumbi wa Mkapa, Mbeya. *Pia zitapatikana kupitia tovuti ya chama: www.umemesaccos.co.tz na zitarejeshwa kupitia barua pepe ya chama info@umemesaccos.co.tz Aidha, uchaguzi wa viongozi unatarajiwa kufanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa 22 wa UMEME SACCOS Ltd, utakaofanyika tarehe 24/10/2026, katika ukumbi uliopo TUGHIMBE HALL, Mbeya Mjini.